HISPANIA WAIFUMUA 4-2 ITALIA NA KUTWAA UBINGWA WA ULAYA U21

IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 3:30 USIKU
KIUNGO Thiago Alcantara amekuwa kivutio katika ushindi wa kikosi cha vijana cha Hispania chini ya miaka 21 wa mabao 4-2 dhidi ya Italia na kutwaa Kombe la Ulaya kwa vijana barani humo, baada ya mchezaji huyo anayetakiwa na Manchester United kufunga mabao matatu mjini Jerusalem.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wa Barcelona amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia Old Trafford.
Alcantara, aliyekuwamo kwenye kikosi cha Hispania kilichoshinda taji hilo miaka miwili iliyopita nchini Denmark, aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya sita, lakini Italia ikasawazisha haraka kupitia kwa Ciro Immobile dakika ya 10.
Thiago akafunga tena dakika ya 31 na 38 kwa penalti, kabla ya Isco kufunga dakika ya 66 kwa penalti pia na Borini akaifungia Italia dakika ya 79 kufanya 4-2.
Kikosi cha Hispania leo kilikuwa; De Gea, Montoya, Bartra, Martinez, Moreno, Koke/Camacho dk86, Illarramendi, Thiago, Tello/Muniain dk70, Morata/Rodrigo dk80 na Isco.
Italy U21; Bardi, Donati, Bianchetti, Caldirola, Regini, Florenzi/Saponara dk58, Rossi, Verratti/Crimi dk76, Insigne, Borini na Immobile/Gabbiadini dk58.Hat-trick hero: Thiago Alcantara netted three goals in the first half to set Spain on their way
Shujaa wa Hat-trick: Thiago Alcantara amefunga mabao matatu kipindi cha kwanza kuipa ushindi Hispania
Group hug: Spain's youngsters celebrate Isco's goal, putting them 4-1 up
Nyota wa Hispania wakishangilia bao la Isco
Despair: Alessandro Florenzi of Italy can't bear to watch as Spain run riot
Alessandro Florenzi wa Italia
Effort: Italy's forward Lorenzo Insigne (left) advances with the ball past Spain's defender Martin Montoya
Lorenzo Insigne wa Italia (kushoto) akimtoka beki wa Hispania, Martin Montoya
Battle: Aberto Moreno of Spain tries to tackle Ciro Immobile of Italy as the Italian advances past
Aberto Moreno wa Hispania akijaribu kumpitia Ciro Immobile wa Italia
Hero: Thiago Alcantara (centre) celebrates his third goal with Cristian Tello (front) and Alvaro Morata
Shujaa: Thiago Alcantara (katikati) akishangilia bao lake la tatu na Cristian Tello (mbele) na Alvaro Morata
Dispute: Giulio Donati, Matteo Bianchetti and Marco Verratti (L-R) appeal against a penalty decision
Kutoka kushoto; Giulio Donati, Matteo Bianchetti na Marco Verratti wakilalamikia penalti
Tussle: Spain forward Cristian Tello (left) challenges Italy's Lorenzo Insigne for the ball
Cristian Tello wa Hispania (kushoto) akikabiliana na Lorenzo Insigne wa Italia
Flying tackle: Spain's Montoya (left) goes straight into a tackle with Vasco Regini of Italy
Montoya wa Hispania (kushoto) akienda chini baada ya kupitiwa na Vasco Regini wa Italia

ULAJI HUOO, KLABU THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA WAKACHEZE ULAYA

Huyu vipi; Mbwana Samatta anacheza TP Mazembe ya DRC, je atakubali kuhamia Thailand ajitengenezee mazingira ya kwenda Ulaya?
Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 12:50 JIONI
KLABU ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza soka nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya.
Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo.
Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport).
Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).
Katika hatua nyingine, TFF inawashukuru washabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa juzi (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwitikio wa washabiki katika mechi hiyo ilikuwa ni moja ya chachu ya kiwango kilichoonyeshwa na Taifa Stars, kwani walishangilia mwanzo hadi mwisho licha ya kupoteza kwa mabao 4-2.
Ni matarajio utakuwepo mwitikio kama huo huo katika mechi ijayo ya Taifa Stars ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) dhidi ya Uganda (The Cranes) itakayochezwa Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu. Stars itaingia tena kambini Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.

MCHEZAJI WA BONGO APATA ULAJI UARABUNI, AOMBEWA ITC AKACHEZE KWA MASLAHI YA MAANA

Wanaongezeka; Thomas Ulimwengu, mmoja wa Watanzania wanaocheza nje, idadi sasa itaongezeka
Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 12:55 JIONI
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania, Gossage Mtumwa ili aweze kucheza soka nchini Yemen.
Mtumwa ambaye anatoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Rollingstone cha Arusha aliombewa hati hiyo na Chama cha Soka Yemen (YFA) kwa ajili ya kucheza nchini humo.
TFF inamtakia kila la kheri Mtumwa katika safari yake ya Yemen, na ni matarajio yetu kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini humo ili wachezaji wengine wa Tanzania nao wapate fursa ya kucheza mpira wa miguu nchini Yemen.
Wakati huo huo: Kamisaa Alfred Kishongole Rwiza ameteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuhudhuria semina ya makamishna itakayofanyika kuanzia Julai 6-7 mwaka huu katika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri.
Semina hiyo inashirikisha baadhi ya makamishna wa CAF walioko kwenye orodha ya makamishna ya shirikisho hilo kwa mwaka 2012-2014.
Rwiza ni mmoja wa makamishna wa CAF kutoka Tanzania, na mechi ya mwisho kusimamia ilikuwa ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa Mei mwaka huu nchini  Msumbiji.
CAF tayari imeshamtumia tiketi Rwiza, na anatarajia kuondoka nchini Julai 4 mwaka huu kwenda Cairo kwa ndege ya EgyptAir.

MABINTI WA KITANGA WATEMBELEA MAPANGO YA AMBONI...SHOO YAO NI JUMAMOSI MKWAKWANI, PATAPENDEZA MAANA TOTOZ NI ZA UKWELI

IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 12:30 JIONI

Washiriki wa shindano la Redd's Miss Tanga 2013, linaloandaliwa na kampuni ya DATK Entertainment, ambalo litafanyika Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakitokeza kwenye moja ya mapango ya Amboni jioni leo, wakati walipotembelea mapango hayo ya kihistoria kujifunza mbalimbali kuhusu mapango hayo. 

Vimwana hao

Totoz kikomandoo

Full Mashauzi..chezea mabinti wa Kitanga weweee

Kwa mapozi sasa...

Mbele ya bango la Amboni

Hapa wanauliza maswali mbalimbali kuhusu mapango hayo, kutoka kwa Ofisa mtoa mwongozo katika mapango hayo

Wamenogaje???

Mahojiano na vyombo vya Habari...

Pozi kwenye mwamba...

Kila aina ya pozi

'WALLAHI' AVB KAWASHIKA PABAYA SPURS...NA HATA REAL WAMUONA BONGE LA 'MCHAWI'

IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 8:40 MCHANA
KOCHA Andre Villas-Boas atataka uhakika juu ya Tottenham kumbakiza Gareth Bale na kupewa fungu la kusajili wachezaji anaowataka kabla ya kujifunga katika klabu hiyo.
Kama ambavyo BIN ZUBEIRY iliripoti wiki iliyopita, Mreno huyo anatakiwa na Paris Saint-Germain akachukue nafasi ya mwalimu anayehamia Real Madrid, Carlo Ancelotti.
Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy anataka kumbakiza kocha wake huyo wa thamani ya juu White Hart Lane msimu ujao.
Crunch time: Andre Villas-Boas wants Tottenham to ensure Gareth Bale stays at the north-London club
Andre Villas-Boas anataka Tottenham imuhakikishie Gareth Bale atabaki Kaskazini mwa London

Lakini Spurs wanafahamu Villas-Boas akienda PSG lazima kocha huyo wa zamani wa Chelsea agharimiwe Pauni Milioni 10 za kuvunja Mkataba.
Wakuu wa Tottenham wanaamini mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 35 anataka kubaki na kukamilisha kazi yake aliyoianza Spurs.
Lakini inafahamika AVB yuko katika nafasi ya kutumia kuhitajiwa kwake na PSG kuushinikiza uongozi utimize matakwa yake majira haya ya joto.
Kuhakikishiwa kubaki kwa Bale, anayetakiwa na PSG na Real Madrid, ndio kipaumbele cha Villas-Boas kipindi hiki, lakini pia anataka kuboresha safu yake ya ushambuliaji.
Crucial: Whether star man Gareth Bale leaves the club could prove decisive in Villas-Boas' future
Hatari: Aidha nyota Gareth Bale abaki ili Villas-Boas abaki, au waondoke wote.

David Villa na Roberto Soldado wote wanahitajiwa, wakati Spurs inammezea mate kwa muda mrefu Leandro Damiao.
And Villas-Boas anataka kuhakikishiwa Levy anafanya jitihada za kuhakikisha anakamilisha mapendekezo yake kabla hajaamua mustakabali wake.
David Villa
Leandro Damiao
Walengwa wakuu: Leandro Damiao (kulia) na mshambuliaji wa Barcelona, David Villa (kushoto) wote wanatakiwa
Killer touch: Roberto Soldado netted during Spain's Confederations Cup victory over Uruguay
Roberto Soldado aliifungia Hispania katika Kombe la Mabara dhidi ya Uruguay

ARSENAL KUMALIZANA NA HIGUAIN WIKI HII, KUSAJILI PIA KINDA LA U-21 YA HISPANIA LINALOITOA UDENDA NA REAL MADRID

IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 2:00 ASUBUHI
KLABU ya Arsenal inatumai kumaliza miaka tisa ya kusubiri saini ya Gonzalo Higuain wiki hii kwa kuweka rekodi ya dau lake la usajili, Pauni Milioni 22 ofa waliyotoa kumnasa mshambuliaji huyo.
BIN ZUBEIRY inafahamu Muargentina huyo amekubali kuhamia Emirates majira haya ya joto na The Gunners - ambao pia wanaamini watambakiza beki Bacary Sagna na Laurent Koscielny kuelekea msimu ujao - wiki hii itafanya mipango rasmi ya kumsaini nyota huyo wa Real Madrid, ambaye ameambiwa yuko huru kuondoka Bernebeu.
On target: Real Madrid striker Gonzalo Higuain could become Arsenal's record signing in a £22m deal
Anatakiwa: Mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain anaweza kuibuka mchezaji ghali kuwahia kusajiliwa Arsenal, kwa Pauni Milioni 22
Watchful eyes: Arsenal boss Arsene Wenger has been reluctant to splash out hefty fees for players in the past
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger yuko tayari kumwaga fedha kusajili

Mazungumzo baina ya viongozi wa Arsenal na wawakilishi wa Higuain yanaendelea vizuri na inasemekana kilichobaki ni klabu hizo mbili kukubaliana.
Kwa sasa dau kubwa la usajili walilowahi kutoa ni Pauni Milioni 15 kwa Zenit St Petersburg kumsajili Andrey Arshavin, Arsenal iko tayari kumpa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki Higuain.
The Gunners imekuwa ikimmezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 tangu akiwa River Plate, timu yake ya kwanza mwaka 2004.
Flop: The disappointing £15m capture of Andrey Arshavin is Arsenal's current record transfer fee
Amechuja: Andrey Arshavin amechemsha Arsenal licha ya kushikilia rekodi ya kusajiliwa bei mbaya

Arsenal ilijaribu uwezekano wa kumsajili Muargentina huyo mzaliwa wa Ufaransa mwaka 2006, lakini wakazidiwa kete na Real Madrid.
Lakini Wenger anatarajiwa kukata kiu yake ya muda mrefu kwa mshambuliaji huyo, Higuain hivi karibuni.
Arsenal imeendelea na nia yake thabiti ya kutaka kuwasajili  Wayne Rooney na Stevan Jovetic, lakini dili la Higuain ndilo la ukweli zaidi.
Young Gun? Arsenal are also lining up a move for Spanish U21 star Asier Illarramendi (centre)
Mtutu mdogo? Arsenal pia inataka kumsajili mchezaji wa U21 ya Hispania, Asier Illarramendi (katikati)

Wakati huo huo, The Gunners wanaongoza mbio ya kuwania saini ya nyota wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Hispania, Asier Illarramendi. 
Kiungo huyo wa ulinzi wa Real Sociedad mwenye thamani ya Pauni Milioni 10 anang'ara kwa sasa na anaitoa udenda na Real Madrid pia. 
Arsenal pia inamfuatilia Gilbert Imbula - lakini Illaramendi akuwa sahihi zaidi akicheza na Mikel Arteta.

LIVERPOOL YAKUBALI 'POTELEA MBALI' SUAREZ, WAMTAKA AWASILISHE BARUA RASMI YA KUOMBA KUONDOKA

IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 1:50 ASUBUHI
KLABU ya Liverpool itamtaka Luis Suarez aandike barua rasmi juu ya nia yake ya kuondoka katika klabu hiyo ili kuamua mustakabali wake.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uruguay, ambaye kwa sasa anacheza Kombe la Mabara, amezungumza mara kadhaa kwenye vyombo vya habari juu ya mpango wake kutaka kuondoka Anfield majira haya ya joto, lakini, bado hajaupa taarifa rasmi uongozi wa Liverpool.
Ikiwa Suarez atauzwa kwa Real Madrid, kama anavyotaka, Liverpool itakubali akiwasilisha barua rasmi ya maombi, wakati pia watataka ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 50. Hadi sasa, Madrid haijawasilisha maombi rasmi ya kutaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
International duty: Luis Suarez has been representing Uruguay
Majukumu ya kimataifa: Luis Suarez anawaikilisha Uruguay

Liverpool bado inafanya mipango ya msimu ujao pamoja na kwamba haijui kama Suarez atabakia, lakini uhalisia ni kwam ba wanajua itakuwa vigumu kumbakiza baada ya matukio yote dhidi yake katika miezi iliyopita.
Ni kwa sababu hizo klabu inataka suala hilo litatuliwe haraka iwezekanavyo.
Kocha Brendan Rodgers, ambaye hadi sasa amemsajili Kolo Toure pekee, anataka kuongeza mabao katika timu yake na Liverpool inataraji kupata uhamisho wa kimataifa saa 24 zijazo kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Celta Vigo, Iago Aspas.
Iago Aspas
Simon Mignolet
Wanaongezwa? Simon Mignolet anatarajiwa kuungana na Iago Aspas Anfield

Aspas anatarajiwa kufuatiwa na winga wa Sevilla, Luis Alberto, wakati mazungumzo yamefikia hatua nzuri kukamilisha usajili wa kipa wa Sunderland, Simon Mignolet. Uhamisho wake ambao unatarajiwa kugharimu Pauni Milioni 10, unaweza kueleweka hadi mwishoni mwa wiki.
Mustakabali wa Andy Carroll baada ya kuomba kuondoka, unatarajiwa kujulikana kabla ya mwishoni mwa wiki.Mshambuliaji huyo wa England, ambaye yupo mapumziko nje, amekubali alifikia makubaliano binafsi na West Ham mwezi uliopita na Liverpool wanataka kumuuza mchezaji huyo kwa Pauni Milioni 15. Kitu kinachotakiwa kwake hivi sasa ni kufaulu vipimo vya afya.
Departing: Andy Carroll is nearing a permanent transfer to West Ham
Anaondoka: Andy Carroll anakaribia kuhamishiwa moja kwa moja West Ham

SUNDERLAND WAMKUBALIA RAIS KIKWETE KUJENGA BONGE LA AKADEMI LA KISASA DAR ES SALAAM

IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 11:30 ALFAJIRI
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mwenyekiti na Mmiliki wa klabu ya Sunderland, Ellis Short na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika akademi ya Light, Sunderland jana mchana. Klabu hiyo kwa ushirikiano na Symbion Power Tanzania Limited imekubali kujenga akademi ya soka mjini Dar es Salaam kufuatia ombi la Rais Kikwete. Rais Kikwete yupo London kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. (Picha zote na Freddy Maro).
Rais Kikwete akizungumza na watoto wanaohudhuria masomo katika shule hiyo. 
Kikwete akizungumza na Mmiliki wa Sunderland, Ellis Short katika Uwanja wa klabu hiyo, Stadium of Light
Rais Kikwete na watoto...Kitu kama hiki kinakuja Dar es Salaam
Rais Kikwete na msafara wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi. Wengine pichani ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Symbion’s Power Limited, Paul Hinks (kushoto), Mbunge wa Ilala, Musa Zungu (wa pili kushoto), Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (wa nne kushoto) na Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka (kulia). 
Rais Kikwete kulia 

SPURS YATAKA KUSAJILI BONGE LA KIUNGO LINALONG'ARA NA BRAZIL KOMBE LA MABARA

IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 11:00 ALFAJIRI
KLABU ya Tottenham inataka kukata Pauni Milioni 15 kwa ajili ya kiungo Mbrazil, Paulinho kupambana na Roma na Inter Milan ili kuinasa saini yake. 
Mpango huo unakuja baada ya Fenerbahce kufufua nia ya kumnunua mshambuliaji Emmanuel Adebayor ambaye atawasaidia kupata fedha.
Paulinho, mwenye umri wa miaka 24, ambaye jina lake kamili ni Jose Paulo Bezerra Maciel Junior, alitarajiwa kusaini kwa moja ya timu za Italia wiki hii baada ya kufikia makubaliano ya awali. 
Highly rated: Paulinho could be on his way to White Hart Lane
Paulinho anaweza kutua White Hart Lane

Pamoja na hayo, nyota huyo wa Corinthians inaelezwa anapenda kuhamia Ligi Kuu ya England.
Tottenham inaweza kutakiwa kupanda dau kidogo hadi Pauni milioni 18 pamoja na kwamba wanahamasika na kujua mchezaji huyo anapenda kuhamia London. 
Akizungumza nchini Brazil, Naibu Mkurugenzi wa Corinthians, Duilio Monteiro Alves, alisema: "(Tottenham) ni klabu ambayo tunafahamu ina nia, lakini bado hakuna kitu rasmi kilichofanyika. Dhahiri itakuja. Tunatarajia siku zijazo.
"Lengo letu ni kumzuia, lakini acha tusubiri na tuone; ikiwa ni nzuri kwake, nzuri kwa Corinthians, tutafanya uamuzi,".
Long-term target: Leandro Damiao has long been linked with Tottenham
Anatakiwa muda mrefu: Leandro Damiao amekuwa akitakiwa kwa muda mrefu Tottenham

Kiungo wa Atletico, Mineiro Bernard, mwenye umri wa miaka 20, pia anatakiwa na mshambuliaji wa Internacional, Leandro Damiao anabaki kuwa suluhisho wakati Mbrazil mwingine, beki kinda wa miaka 18 wa Botafogo, Doria, amekuwa akijadiliwa.
Paulinho amezivutia Roma, Inter na Tottenham, lakini amesema hatatoa uamuzi hadi baada ya Kombe la Mabara. 
Kuwasili kwake White Hart Lane kutafungua milango ya watu kuondoka Spurs, kama inavyofahamika Fulham inamtaka Tom Huddlestone na mkongwe mwenye umri wa miaka 32, Scott Parker, ambaye anatakiwa Sunderland.
Tom Huddlestone
Scott Parker
Wanaondoka? Tom Huddlestone na Scott Parker wanaweza kuondoka Tottenham
Departing? Emmanuel Adebayor could be sold by Spurs
Anaondoka? Emmanuel Adebayor anaweza kuuzwa Spurs

Adebayor ni kati ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi katika klabu hiyo na kuondoka kwake kutasaidia kufanikisha kwa dili nyingine. 
Fenerbahce ilijaribu kumsaini mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 29 kabla wakati akiwa bado Manchester City na inatarajia kufanikisha mpango wake safari hii.

NIGERIA YAFANYA MAUAJI KOMBE LA MABARA, YAWAFUMUA MABINGWA WA OCEANIA 6-1

IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 6:20 USIKU
TIMU ya taifa ya Nigeria imeifumua kwa mabao 6-1 Tahiti katika Kombe la Mabara usiku huu.
Jonathan Tehau aliifungia Tahiti, lakini Nnamdi Oduamadi akaifungia Super Eagles mabao matatu peke yake.
Mabingwa wa Oceania, Tahiti, wakiwa na mchezaji mmoja tu wa kulipwa kikosini, walikuwa wana mwanzo mgumu katika mchezo huo wa Kundi B wakati mpira ulipomgonga refa na kumkuta mchezaji wa Nigeria, Uwa Echiejile ambaye alifunga kwa shuti la kubabatiza dakika ya tano.
Nigeria ikapata bao la pili lililofungwa na Oduamadi dakika tano baadaye.
Tahiti iliwanua vitini mashabiki wake wakati Tehau alipofunga bao dakika ya 54.
Lakini Nigeria iliendelea kung'ara wakati Tehau alipojifunga kabla ya Oduamadi kukamilisha Hat-trick yake na Echiejile akafunga bao lake la pili kwenye mchezo huo.
Kikosi cha Nigeria kilikuwa: Enyeama, Ambrose, Omeruo, Oboabona, Echiejile, Ogude, Mikel, Mba, Oduamadi, Ujah na Musa.
Tahiti: Samin, A Tehau, Vahirua, Ludivion, Caroine, Bourebare, Vallar, Chong Hue, Aitamai, J Tehau na Simon.
On target: Nnamdi Oduamadi (right) celebrates after scoring against Tahiti
Nnamdi Oduamadi (kulia) akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Tahiti
Tucked away: Nnamdi Oduamadi of Nigeria scores his team's second goal
Nnamdi Oduamadi wa Nigeria akifunga
One for the underdog: Jonathan Tehau rose to nod home a goal for Tahiti
Jonathan Tehau akiifungia Tahiti
One for the underdog: Jonathan Tehau rose to nod home a goal for Tahiti
Jonathan Tehau akifunga
Party time: Even though they were losing, Tahiti celebrated their goal wildly
Anashangilia
Tehau
Tehau
Tehau
Five star: Oduamadi scores the fifth goal for his country as Tahiti collapsed
Oduamadi akifunga bao la tano
Nigeria 
Salute: Tahiti players acknowledge the support of their fans, including the chaps below, after the game
Saluti: Wachezaji wa Tahiti 
LET'S GO TAHITI