• HABARI MPYA

    Thursday, July 31, 2014

    MAKOCHA WA BARCELONA WAWASILI DAR TAYARI KUTOA MAFUNZO KWA MAKOCHA WA TANZANIA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    BIA ya Castle Lager, bia inayoongoza barani Afrika na FC Barcelona, moja kati ya timu kubwa zaidi za soka duniani wameshirikiana kuleta makocha kutoka klabu hiyo yenye makao yake huko Camp Nou, Hispania ili kutoa mafunzo ya mbinu za soka kwa makocha wa Tanzania wiki hii. Makocha hao wa FC Barcelona ambao wataendesha mafunzo hayo wamefika jijini Dar es salaam leo (31/8/2014). 
    Mafunzo hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kwa siku mbili zijazo ambazo ni tarehe 1 na tarehe 2 Agosti na yataendeshwa na makocha waliobobea kwenye mbinu mbalimbali za kandanda ikiwemo Tiki Taka.
    Makocha hawa ni Daniel Bigas Alsina and Isaac Oriol Guerrero Hernandez kutoka Shule ya Soka ya FB Barcelona.
    Mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano uliosainiwa mwaka jana kati ya FC Barcelona na Castle Lager ambayo ni bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika. Vilevile, mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano huu kwa jamii. 
    Kupitia mafunzo haya, makocha 30 waliobahatika kutoka ligi kuu na ligi daraja la kwanza watapata fursa maalum ya kujifunza mbinu mbalimbali za mazoezi zinazotumiwa na FC Barcelona na kufanikiwa kuwatengeneza baadhi ya wachezaji wenye mafanikio makubwa zaidi duniani. 
    “Tuna shauku kubwa sana kuona mafunzo haya yanakuja Tanzania na tunafurahia kupata nafasi ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inatuunga mkono. Tunaamini mafunzo haya yatawanufaisha makocha na wachezaji wa Tanzania katika siku zijazo,” alisema Fimbo Buttallah, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania.
    “Castle Lager ina historia kubwa na soka barani Afrika na tukio hili litazidi kuimarisha uhusiano uliopo kati ya bia namba moja Afrika na mchezo namba moja kwa kupendwa barani Afrika.”
    Mafunzo haya kwa makocha yatahusisha mafunzo ya darasani kwa nadharia na uwanjani kwa vitendo.  Ikiwa ni sehemu ya mafunzo hayo, makocha hao watatoa baadhi ya siri za mafanikio ya FC Barcelona ili kusaidia kuleta utaalamu wa kimataifa kwenye soka la Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAKOCHA WA BARCELONA WAWASILI DAR TAYARI KUTOA MAFUNZO KWA MAKOCHA WA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top