• HABARI MPYA

    Thursday, August 21, 2014

    AZAM FC ILIVYOIPA MKONO WA KWAHERI MICHUANO YA KAGAME JANA KIGALI

    Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbangu kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki wa El Merreikh ya Sudan, Gabir Abdu Mohamed katika mchezo wa Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame jana Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda. Merreikh ilishinda kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
    Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar (katikati) akitafuta mbinu za kumpokonya mpira kiungo wa Merreikh, Amir Kamal kushoto
    Beki wa Azam FC, Erasto Nyoni kushoto akimtoka beki wa Merreikh, Ayman Said Mohammed
    Kiungo wa Azam FC, Himid Mao akimiliki mpira mbele ya beki wa Merreikh, Ali Gaffer Hussein, huku mwenzake Didier Kavumbangu akiwa tayari kutoa msaada 
    Salum Abubakar 'Sure Boy' akiwania mpira wa juu na mchezaji wa Marreikh, Ali Gaffer Hussein
    Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akidhibitiwa na beki wa Marreikh Ali Gaffer Hussein
    Sure Boy na Ali Gaffir Hussein ilikuwa shughuli pevu jana katikati ya Uwanja 
    Mshambuliaji wa Azam FC, Leonel Saint- Preux akipasua katikati ya wachezaji wa Merreikh
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC ILIVYOIPA MKONO WA KWAHERI MICHUANO YA KAGAME JANA KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top