• HABARI MPYA

    Thursday, August 21, 2014

    DZEKO ASAINI MKATABA MPYA MAN CITY HADI 2018

    MSHAMBULIAJI Edin Dzeko amesaini Mkataba wa miaka minne na mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City. 
    Mwanasioka huyo wa kimataifa wa Bosnia ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter juu ya kusaini kwake mkataba mpya akisema: "Furaha na kujivuniaa kusaini mkataba wangu mpya na Manchester City. Nipo hapa ambako ni kwangu. Nimerefusha hadi 2018,". 
    Mpachika mabao huyo amefunga mara 65 katika mechi 156 alizoichezea klabu hiyo tangu ajiunge nayo kutoka Wolfsburg mwaka 2011. 
    Anamwaga wino: Edin Dzeko amesaini mkataba mpya wa miaka minne Manchester City
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DZEKO ASAINI MKATABA MPYA MAN CITY HADI 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top