• HABARI MPYA

    Friday, August 01, 2014

    ELIAS MAGURI AANGUKA MIAKA MIWILI SIMBA SC

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa Ruvu Shooting, Elias Maguri amesaini Mkataba wa miaka miwil kujiunga na Simba SC.
    Maguri aliyechezea Prisons ya Mbeya awali, amesema; “Kutua Simba SC ni ndoto yangu ya muda mrefu sana tangu nipo mdogo nilikuwa ninaota kuchezea timu kubwa,”.
    Aidha Maguri akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya kumalizana na Simba SC, amesema kwamba anafahamu changamoto inayomkabili baada ya kusaini timu hito kubwa na amejiandaa vyema kukabiliana nayo.
    Ametua Msimbazi; Elias Maguri amesaini miaka miwili Simba SC

    “Simba SC ni timu kubwa na ina wachezaji wakubwa, wa hapa hapa nyumbani na wa kigeni pia, yote ninayajua na kwa kuwa najiamini ndiyo maana sikusita kusaini,”amesema.
    Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba mshambuliaji huyo ni kijana mdogo ambaye wanaamini atakuwa na wakati mzuri kwenye klabu yao.
    “Maguri bado ni kijana mdogo, akiwa Simba SC atakuwa na fursa nzuri ya kuongeza ujuzi na uzoefu wake kisoka,”amesema.
    Maguri kushoto akisaini na Kaburu leo Msimbazi

    Kipaji hicho kutoka mkoani Mara kilichototokea kwenye mtandao wa mashindano ya vijana ya Copa Coca Cola, msimu uliopita kilikuwemo kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen.
    Januari mwaka huu alikwenda Oman kujaribu kujiunga na Seeb ya Ligi Kuu ya huko, lakini akafeli majaribio. 
    Aliporejea nchini, aliingia kwenye mtafaruku na klabu yake, Ruvu Shooting kwa kuondoka bila kuaga, kabla ya kumalizana na kuendelea kucheza.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ELIAS MAGURI AANGUKA MIAKA MIWILI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top