• HABARI MPYA

    Wednesday, August 20, 2014

    JULIO CESAR ATUA BENFICA MIAKA MIWILI BAADA YA KUPOTEZA NAMBA QPR

    KLABU ya Benfica imekamilisha usajili wa kipa wa kimataifa wa Brazil, Julio Cesar kwa mkataba wa miaka miwili kutoka QPR.
    Mlinda mlango huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na klabu hiyo ya London mwaka 2012, lakini akacheza mechi 24 kabla ya kwenda kwa mkopo Toronto.
    Robert Green amechukua nafasi yake kama kipa wa kwanza wa klabu hiyo na Benfica imeamua kumchukua kipa huyo aliidakia Brazil iliyofanya vibaya Kombe la Dunia mwaka huu.

    Namba moja: Julio Cesar sasa atacheza Ligi ya Mabingwa baada ya kusaini Benfica ya Ureno
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JULIO CESAR ATUA BENFICA MIAKA MIWILI BAADA YA KUPOTEZA NAMBA QPR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top