• HABARI MPYA

    Wednesday, September 17, 2014

    BALOTELLI AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO LIVERPOOL IKIUA 2-1 ULAYA

    LIVERPOOL imerudi vizuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya usiku huu kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Ludogorets Uwanja Anfield.
    Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli amefunga bao lake la kwanza leo Liverpool dakika ya 81, kabla ya Dani Abalo kuisawazishia Ludogorets.
    Nahodha Steven Gerrard aliihakikishia Liverpool kushinda mechi ya kwanza ya makundi kwa bao la penalti dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Lovren, Sakho, Moreno, Henderson, Gerrard, Lallana/Borini dk67, Sterling, Coutinho/Lucas dk67 na Balotelli.
    Ludogorets: Borjan, Caicara, Moti, A Aleksandrov, Minev, Dyakov, Abel, M Aleksandrov, Marcelinho, Misidjan na Bezjak. 
    Mario Balotelli celebrates opening his Liverpool account
    Balotelli broke the deadlock late in the second half
    Mario Balotelli akishangilia baada ya kuifungia Liverpool
    Mario Balotelli amefunga bao lake la kwanza leo Liverpool ikianza na ushindi Ligi ya Mabingwa Ulaya
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALOTELLI AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO LIVERPOOL IKIUA 2-1 ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top