• HABARI MPYA

    Monday, September 01, 2014

    CHICHARITO AFAULU VIPIMO VYA AFYA, RASMI NI MCHEZAJI WA REAL MADRID

    MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amekamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Real Madrid pamoja na uwezekano wa kununuliwa moja kwa moja kutoka Manchester United baadaye.
    Real inamchukua mchezaji huyo baada ya kufaulu vipimo vya afya leo mjini Madrid.
    United inataka dau la Pauni Milioni 17 kumuuza moja kwa moja mchezaji huyo, lakini kwa mkataba wa sasa wa mkopo wa muda mrefu wa msimu, Louis van Gaal anachukua Pauni Milioni 1.5.
    United imethibitisha katika ukurasa wake wa Twitter leo kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo kwenda Real Madrid. 

    Ameondoka: Javier Hernandez ametua Real Madrid kwa mkopo 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHICHARITO AFAULU VIPIMO VYA AFYA, RASMI NI MCHEZAJI WA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top