• HABARI MPYA

    Tuesday, September 16, 2014

    MAAFANDE WA KIPANGA WAIKOSAKOSA MIEMBENI KUDUCHU TU

    Na Ameir Khalid, ZANZIBAR
    WAKONGWE wa soka visiwani Zanzibar timu ya Miembeni SC, jana bado kidogo waripuliwe na mizinga ya maafande wa Kipanga katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar Grand Malt iliyoingia siku ya pili leo.
    Miembeni walilazimika kusubiri dakika ya 89 kujipatia bao la kusawazisha baada ya kuwa nyuma kwa bao 1-0 mbele ya lililofungwa na mchezaji Abubakar Ayoub dakika nne kabla mapumziko kufuatia wachezaji wa Kipanga kugongeana mpira kabla kumkuta mfungaji aliyeujaza kimiani.

    Wachezaji wa Miembeni (jezi nyeupe) na wa Kipanga wakipambana leo Uwanja wa Amaan.

    Othman Omar ndiye aliyeikomboa Miembeni SC na kuifanya itoke na pointi moja baada ya kusawazisha bao hilo kufutia mpira wa adhabu uliopanguliwa na kipa wa Kipanga Salum Hassan na kisha kubaki kwenye eneo la goli lake ukileta piga nikupige hadi Omar akaukwamisha nyavuni.
    Kesho katika uwanja wa Amaan kutakuwa na shughuli pevu wakati mabaharia wa KMKM ambao ndio  mabingwa watetezi watakapoumana na wakongwe wengine wa ligi hiyo, Malindi SC.
    Nao uwanja wa Gombani Pemba utaanza mechi ya kwanza msimu huu kwa pambano kati ya maafande wa Polisi na wanajeshi wengine, Hard Rock wanaomilikiwa na JWTZ kisiwani Pemba.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAAFANDE WA KIPANGA WAIKOSAKOSA MIEMBENI KUDUCHU TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top