• HABARI MPYA

    Wednesday, September 17, 2014

    TEVEZ BADO MOTO, APIGA ZOTE MBILI JUVE IKIUA 2-0 ULAYA, ATLETICO 'WASULUBIWA' UGIRIKI

    MABAO mawili ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Muargentina Carlos Tevez usiku huu yameipa ushindi wa 2-0 Juventus ya Italia katika mchezo wa makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Tevez aliyewahi pia kuchezea Manchester City, alifunga bao moja kila kipindi dhidi ya Malmo FF ya Sweden katika dakika za 59 na 90 na kukipa mwanzo mzuri Kibibi Kizee cha Turin katika michuano hiyo mikubwa zaidi ya klabu barani Ulaya.
    Wana fainali wa michuano ya msimu uliopita, Atletico Madrid wamepata kipigo cha ugenini kutoka kwa Olympiacos ya Ugiriki cha mabao 3-2.
    Mabao ya wenyeji yamefungwa na Arthur Masuaku dakika ya 13, Ibrahim Affelay dakika ya 31 na Mitroglou dakika ya 74 wakati ya wageni yamefungwa na Mario Mandzukic dakika ya 38 na Griezmann dakika ya 87.
    Carlos Tevez bado moto, amefunga zote mbili Juve ikiua 2-0 Ulaya
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TEVEZ BADO MOTO, APIGA ZOTE MBILI JUVE IKIUA 2-0 ULAYA, ATLETICO 'WASULUBIWA' UGIRIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top