• HABARI MPYA

    Tuesday, September 02, 2014

    YANGA SC WAIKIMBIA SIMBA POSTA

    YANGA SC imevunja Mkataba wa kupitishia malipo ya ada za wanachama wake Benki ya Posta na kuingia Mkataba mpya wa aina hiyo na beki ya CRDB.
    Viongozi wa Yanga SC na CRDB wanakutana na Waandshi wa Habari muda huu kutangaza ndoa yao hiyo mpya baada ya klabu hiyo kuachana na benki ya Posta waliyoingia nayo Mkataba Juni mwaka huu.
    Sababu za Yanga kufikia uamuzi huo, ni baada ya kuona benki ya Posta imeshindwa kuwafanya wafikie malengo yao waliyojiwekea na kwamba katika mkataba wao, kulikuwa kuna kipengele cha kuuvunja iwapo malengo hayatafikiwa. Benki ya Posta iliingia Mkataba wa aina hiyo na Simba SC pia. TAARIFA ZAIDI ITAFUATIA.
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga mkataba wa makabaliano yao kuhusu kuanzishwa kwa akaunti ya mashabiki na wanachama wa klabu hiyo katika hafla iliyofanyika Hyatt Regency jijini Dar es Salaam Juni mwaka huu. Ndoa hiyo imevunjika ndani ya miezi mitatu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAIKIMBIA SIMBA POSTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top