• HABARI MPYA

    Tuesday, September 02, 2014

    ZENGWE USAJILI WA FALCAO, MAN UNITED YADAIWA KUMSAJILI NJE YA MUDA

    ZENGWE. Manchester United inadaiwa kubebwa katika usajili wake, baada ya kukiuka kanuni hususan katika usajili wa mshambuliaji Radamel Falcao. 
    Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeandika kwamba, Falcao amesajiliwa baada ya dirisha la usajili kufungwa Saa 5:00 usiku jana- wakati beki Marcos Rojo pamoja kusajiliwa mapema, lakini bado hajapatiwa visa ya kufanyia kazi.
    Inaelezwa Jumatatu ndiyo pazia la usajili limefungwa, lakini hadi Saa 5:00 usiku uhamisho wa Falcao ulikuwa haukamilika. 
    Sheria za usajili zinasema usajili wote uwe umekamilishwa ifikapo Saa 5:00 usiku wa kufungwa pazia na baada ya hapo, vielelezo vyote kama mikataba, makubaliano ya uhamisho na vibali vya kufanyia kazi Uingereza lazima viwasilishwe.
    Sheria imefuatwa?
    Ligi Kuu ya England inaruhusu saa mbili, huo ni uamuzi wao – lakini uhamisho wa kimataifa lazima uaendane na mfumo wa FIFA wa elektroniki (TMS) kufungwa usiku huo.
    Mfumo wa FIFA wa TMS ni wa mtandao ambao unatoa fursa kwa data zote muhimu kuingizwa ili kuweka sawa uhamisho wa kimataifa.
    Angalau usajili wa Rojo wa Pauni Milioni 16 kutoka Sporting Lisbon umekamilika katika masuala ya kisoka. Amepewa hati ya kimataifa na Chama cha Soka na aliwasili England wiki iliyopita kukamilsha dili lake.
    Lakini sheria za uhamiaji zinasema wachezaji wanaoingia nchini humo, lazia wawe na visa za kufanyia kazi.
    Na maofisa wa Ubalozi kwanza watafuatilia madai ya kwamba kukwama kwa visa yake kunatokana na ugomvi baina yake na jirani yake nchini kwao, Argentina mwaka 2010 kabla ya kumpatia visa ya kufanyia kazi, huku tukio hilo bado linachunguzwa na Polisi.
    Lakini wakati wachezaji wa Man United wamepitishwa pamoja na kuwa nje ya muda au kukwama kwenye baadhi ya mambo ya msingi katika usajili wao, wachezaji wengine wamekwamishwa na hapo ndipo Daily Mail wanapouliza haki wapi?
    Had Van Gaal gone to bed? Falcao poses with Manchester United assistant manager Ryan Giggs
    Usajili batili? Usajili wa Falcao inadaiwa umefanyika baada ya pazia kufungwa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZENGWE USAJILI WA FALCAO, MAN UNITED YADAIWA KUMSAJILI NJE YA MUDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top