• HABARI MPYA

    Sunday, October 19, 2014

    CHELSEA KUMKOSA DIEGO COSTA LIGI YA MABINGWA, MOURINHO ASEMA KURUDI UWANJANI LABDA NOVEMBA KATIKATI

    MSHAMBULIAJI Diego Costa ataukosa mchezo wa Jumanne wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu yake Chelsea ikimenyana na NK Maribor Uwanja wa Stamford Bridge, amesema kocha Jose Mourinho. 
    Costa alikuwa nje ya kikosi cha Chelsea jana kikishinda 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu ya England na ataendelea kupata tiba kwa muda.
    Mpachika mabao huyo wa zamani wa Atletico Madrid aliumia akiichezea timu yake ya taifa Hispania na Mourinho amesikitishwa mno na kumkosa nyota wake huyo mkali wa mabao. 
    Diego Costa atakosekana Chelsea ikicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya keshokutwa

    "Baada ya mechi na Arsenal akaenda timu ya taifa, akacheza mechi mbili kubwa na amerudi akiwa na hali ambayo hawezi kucheza,"amesema Mourinho.
    "Nafikiri atakuwa katika hali nzuri katikati ya Novemba kurejea katika timu ya taifa. Tutakuwa makini mno juu yake. Atacheza kwangu atakapokuwa huru baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa,"amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA KUMKOSA DIEGO COSTA LIGI YA MABINGWA, MOURINHO ASEMA KURUDI UWANJANI LABDA NOVEMBA KATIKATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top