• HABARI MPYA

    Tuesday, October 21, 2014

    DI MARIA AZUA HOFU MAN UNITED

    WINGA Angel di Maria alionekana hayuko vizuri akiwa ameketi kwenye benchi la Manchester United usiku wa jana, huku amekandamizia barafu katika nyonga yake kwenye mchezo huo ulioisha kwa sare ya 2-2 na West Bromwich Albion.
    Muargentina huyo, aliyesajiliwa kwa dau la rekodi United, alikuwa kivutio Uwanja wa The Hawthorns, lakini kulikuwa kuna wasiwasi juu ya kiungo huyo baada ya kutolewa dakika ya 76.
    Di Maria amekuwa katika kiwango babu kubwa tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 60 kutoka Real Madrid msimu huu na ameendeleza mwanzo wake mzuri usiku wa jana. 

    Angel Di Maria akitoka uwanjani anachechemea jana
    Di Maria (right, sat down), holds an ice pack on his groin as Chris Smalling, Ander Herrera and Ryan Giggs look over at the Manchester United star in the dugout at the Hawthorns
    Di Maria (aliyekaa chini kulia) akiwa amekandamizia barafu kwenye nyonga yake huku Chris Smalling, Ander Herrera na Ryan Giggs wakimuangalia kwenye benchi jana Uwanja wa The Hawthorns

    Alimsetia Marouane Fellaini kufunga bao la kusawazisha kipindi cha pili, kabla ya kumpisha Ashley Young. Amecheza mechi tano hadi sasa Manchester United na amefunga mabao matatu na kusaidia manne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DI MARIA AZUA HOFU MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top