• HABARI MPYA

    Sunday, October 19, 2014

    MADUDU YA BODI YA LIGI YASABABISHA VODOCOM ‘KUFANYA DHULUMA’ LIGI KUU, TUZO ZA MEXIME NA KAVUMBANGU WAPEWA MATOGOLO NA MWAMBUSI

    Na Mahmoud Zubeiry, MBEYA
    MAKOSA ya Bodi ya Ligi, jana yameisabisha Vodacom Tanzania, wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara kufanya dhuluma bila kutarajia.
    Vodacom jana imetoa tuzo kwa Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba Anthony Matogolo na Kocha Bora wa Mwezi, Juma Mwambusi, kila mmoja akipewa Sh. Milioni 1.
    Lakini hiyo inafuatia makosa ya Bodi ya Ligi chini ya Mtendaji wake Mkuu, Silas Mwakibinga kuwateua wawili hao kuwa Mchezaji na Kocha Bora wa Septemba wakati hawakustahili.
    Tuzo ya Mchezaji Bora wa Septemba kwa mujibu wa takwimu za kitaalamu ilistahili kwenda kwa mshambuliaji wa Azam FC, Mrundi Didier Kavumbangu wakati Kocha Bora alistahili kupewa Mecky Mexime wa Mtibwa Sugar ya Morogoro.
    Katika mwezi Septemba, kila timu ilicheza mechi mbili Ligi Kuu na Mbeya City ilitoa sare moja ya bila kufungana nyumbani na kushinda moja, wakati Mtibwa ilishinda zote, ikiwemo dhidi ya vigogo Yanga SC.
    Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Dk Norman Sigella akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Miliomi 1 mchezaji wa Mbeya City, Anthony Matogolo Uwanja wa Sokoine jana, baada ya kutajwa na Bodi ya Ligi kimakosa kuwa Mchezaji Bora wa Septemba

    Mechi ambayo Mbeya City ilishinda, ilikuwa ni bao 1-0 tena kwa penalti, wakati Mtibwa Sugar na Azam FC zilishinda mechi zote na hadi sada zinaongoza Ligi Kuu kwa kila timu kuwa na ponti 10, huku MCC imekwamia kwenye pointi tano. Kavumbangu alifunga mabao manne ndani ya Septemba na akatoa pasi ya bao moja kati ya mabao sita ambayo Azam ilivuna kwenye mechi zake mbili za kwanza mwezi huo.
    Kitaalamu, hawa ndiyo walistahili kupata tuzo za Septemba, lakini kwa makosa ya Bodi ya Ligi wamedhulumiwa haki zao na kupewa watu ambao hawakustahili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MADUDU YA BODI YA LIGI YASABABISHA VODOCOM ‘KUFANYA DHULUMA’ LIGI KUU, TUZO ZA MEXIME NA KAVUMBANGU WAPEWA MATOGOLO NA MWAMBUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top