• HABARI MPYA

    Monday, October 20, 2014

    MALINZI ATAKA KLABU ZIKUTANE KUJADILI NAMNA YA KUCHANGIA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezitaka klabu kukutana na kujadili namna ya kuchangia mfuko wa maendeleo ya vijana.
    TFF ilikutana na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) mwishoni mwa wiki na kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha maendeleo ya mchezo huo nchini.
    Mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam uliongozwa na Rais wa TFF, Malinzi na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF pamoja na Wenyekiti wa klabu za VPL.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi kushoto

    Mbali na suala hilo, pia kikao hicho kilizungumzia leseni za klabu (club licensing), maboresho ya Taifa Stars, Kanuni za Ligi Kuu, Kombe la FA (Shirikisho) na mchango wa klabu hizo katika kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana.
    Uwasilishaji katika mkutano huo kuhusu maboresho ya Taifa Stars ulifanywa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mart Nooij wakati leseni kwa klabu ulifanywa na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura.
    Kuhusu Kombe la FA, klabu zilifahamishwa kuwa mazungumzo kati ya TFF na mdhamini yanaendelea, ambapo zilikaribisha wazo hilo kwa vile michuano hiyo itatoa fursa kwa timu zao kucheza mechi nyingi za mashindano, hivyo kutoa nafasi ya kucheza kwa wachezaji wengi zaidi.
    Bingwa wa michuano ya FA ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
    Rais Malinzi aliziomba klabu kukutana na kuwasilisha mapendekezo yao ya jinsi ya kuchangia/kuboresha maendeleo ya mpira wa miguu kwa vijana, kuboresha Kanuni za Ligi Kuu na kuboresha Kanuni za Bodi ya Ligi ili yaweze kufanyiwa kazi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI ATAKA KLABU ZIKUTANE KUJADILI NAMNA YA KUCHANGIA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top