WAHENGA walisema, mwenye nacho huongezewa- usemi huo unadhihirika kwa mara nyingine kupitia bondia Floyd Mayweather Jnr ambaye kishinda kitita ch fedha baada ya kubeti kwenye mchezo wa NFL.
Bingwa huyo wa madaraja matano tofauti ya uzito wa ndondi duniani, ambaye tayari ni mwanamichezo tajiri ulimwenguni, sasa ameshinda kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 4 katika beti zake za wiki za karibuni.
Mafanikio mapya ya Mayweather yanakuja baada ya kuweka dola 800,000 katika mchezo ambao Arizona Cardinals imeifunga Oakland Raiders.
Risiti za Mayweather katika kubeti ambazo zimemuingizia mamilioni ya dola
Cardinals ilishinda 24-13, maana yake Mayweather amevunja zaidi ya cola Milioni 1.5 na kama kawaida yake, 'Mtu Fedha' huyo akaposti kwenye akaunti yake ya Twitter kusherehekea mafanikio hayo pamoja na watu Miloni 5.34 wanaomfolo.
Mayweather aliingiza cola Milioni 105 katika pambano lake na Saul Alvarez na la ushindi wake wa kwanza dhidi ya Marcos Maidana na sasa anajiandaa kwa pambano lingine Mei, mwakani.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 amebakiza mapambano mawili katika Mkataba wake wa mapambano sita na Showtime na amesema baada ya halo atastaafua. Moja ya mapambano yake mawili linatarajiwa kuwa dhidi ya Muingereza Amir Khan mjini Las Vegas Mei mwakani.
Arizona Cardinals wakishangilia ushidi wao dhidi ya Oakland Raiders ambao umempoa fedha Mayweather
0 comments:
Post a Comment