• HABARI MPYA

    Sunday, October 19, 2014

    RONALDO KWA MABAO ACHANA NAYE, APIGA MBILI REAL IKIUA 5-0 LA LIGA

    KLABU ya Real Madrid imeifumua mabao 5-0 Levante na kusogea nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga, ikizidiwa pointi nne na vinara, Barcelona
    Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili, kwanza la penalti dakika ya 13 na la tatu dakika ya 61, sasa akifikisha mabao 15 msimu huu katika ligi hiyo baada ya mechi mechi saba.
    Mabao mengine ya Real, yamefungwa na Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 38, James Rodriguez dakika ya 66 na Isco dakika ya 82.
    Kikosi cha Real kilikuwa; Casillas, Carvajal, Pepe, Nacho, Marcelo/Arbeloa dk73, Rodriguez, Modric/Medran dk79, Kroos/Illarramendi dk68, Isco, Hernandez na Ronaldo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO KWA MABAO ACHANA NAYE, APIGA MBILI REAL IKIUA 5-0 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top