• HABARI MPYA

    Tuesday, November 18, 2014

    MTIBWA SUGAR YAWAITA SIMBA SC WAJIBEBE NYOTA WATAKAO, YAWAAMBIA; “HELA YENU TU”

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MTIBWA Sugar imesema iko tayari kuwauza wachezaji wake wawili wanaowaniwa na Simba SC, beki Kessy Hamisi na mshambuliaji Ame Ali- kwani si sera yao kuwabania wachezaji.
    Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Meck Mexime ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mchezaji yeyote anayetaka kuondoka katika timu hiyo hawezi kuzuiwa, ili mradi taratibu zimefuatwa.
    “Sisi siyo sera yetu kuwabania wachezaji, nadhani timu zote zinajua, hawa wachezaji wote wana mikataba hapa, klabu inayowataka iende kwa uongozi tu,”amesema Mexime.
    Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime

    Wawili hao wameng’ara na Mtibwa Sugar katika mechi saba za awali za Ligi Kuu, wakiiwezesha timu hiyo kuwa kileleni na baada ya hapo, wamezivutia timu nyingine nchini.
    Ame amefunga mabao manne katika mechi hizo na kuingia kwenye mbio za kuwania ufungaji bora wa Ligi Kuu, akichuana na Mrundi, Didier Kavumbangu wa Azam FC. 
    Simba SC inataka kuboresha kikosi chake kabla ya Ligi Kuu kurudi tena mwishoni mwa mwezi ujao, baada ya mapumziko mafupi tangu wiki iliyopita.
    Na tayari inaelezwa miongoni mwa wachezaji ambao inawataka ni nyota hao wawili wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, mabingwa wa Ligi Kuu 1999 na 2000. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAWAITA SIMBA SC WAJIBEBE NYOTA WATAKAO, YAWAAMBIA; “HELA YENU TU” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top