• HABARI MPYA

    Sunday, March 01, 2015

    FABIOLA ACHUKUA DHAHABU KILI MARATHON 2015

    NA Mohammed Mharizo, MOSHI
    MWANARIADHA wa Tanzania Fabiola William (32),ameibuka mshindi wa kilomita 42 (Full Marathon) katika mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika jana mjini hapa na kujinyakulia Sh milioni 4 baada ya kutumia 2:49:51.
    Nafasi ya pili ilichukuliwa na Rosaline David (Kenya) aliyetumia 2:50:39 na kujinyakulia Sh milioni mbili wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Joan Cherop (Kenya) alitumia 2:50:44 na kujinyakulia Sh milioni moja.

    Fabiola William akimalizia kwa furaha mbio za Kili Marathon 

    Nafasi ya nne ilikwenda kwa Dorice Todipus (Kenya), aliyetumia 2:53:17 na kujinyakulia Sh laki saba wakati nafasi ya tano ilikwenda kwa Sarah Maiyo (Kenya), nafasi ya sita alichukua Gladys Cheruiyo (Kenya), nafasi ya saba ni Susan Koskei (Kenya),  nafasi ya nane ni Julitter Tanin (Kenya), nafasi a tisa ni Esther Mutuku (Kenya) na nafasi ya kumi ni Lilian Chelimo (Kenya).
    Kwa upande wa Full Marathon wanaume, David Ruto (Kenya), aliibukamshindibaada ya kutumia 2:15:50 na kuzawadiwa Sh milioni 4 huku wa pili akiwa ni Benard Kimayo (Kenya) aliyetumia 2:15:52 na kuzawadiwa Sh mbili na wa tatu ni Alex Bartida aliyetumia 2:16:00 na kujizolea Sh milioni moja.
    Nafasi ya nne alishika George Ngure (Kenya), huku Douglas Chebii (Kenya) alishika nafasi ya tano, nafasi ya sita ni Pascal Mombo (Tanzania), nafasi ya saba ni David Kilimo (Kenya), Lawrence Rotich (Kenya) alishikanafasi ya nane huku nafasi ya tisa ikienda kwa Mathew Koskei (Kenya) na nafasi ya kumi ni Siegried Ngolly (Tanzania).

    Mshindi wa Nusu Marathon (Kilomita 21) wanawake, Grace Kimanzi wa Kenya akipokea zawadi yake

    Kwa upande wa Half Marathon Kiloimita 21 wanaume,  Ismael Juma (Tanzania), aliibuka mshindi baada ya kutumia 1:03:05 na kujinyakulia Sh milioni 2 huku nafasi ya pili ikienda kwa Emmanuel Giniki (Tanzania), aliyetumia 1:03:15 na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Theotil Joseph (Tanzania), aliyetumia 1:03:25.
    Nafasi ya nne ilikwenda kwa Felix Alfonse (Tanzania), nafasi ya tano Festus Stalamestus (Kenya), nafasi ya sita ni Vicent Kipruto (Kenya), nafasi ya saba ni Fanuel Mkungo (Kenya), nafasi ya nane ni Dickson Kimuthi (Kenya), nafasi ya tisa ni Elia Sidame (Tanzania) na nafasi ya kumi ni Martin Muhinde (Kenya).
    Kwa upande wa Half Marathon Kilomita 21 wanawake, Grace Kimanzi (Kenya), aliibuka mshindi wa kwanza baada ya kutumia 1:12:35 na kujinyakulia Sh milioni 2 huku nafasi ya pili ikienda kwa Yunice Echumba (Kenya), aliyetumia 1:12:52 na kujizolea Sh milioni moja na nafasi ya tatu alishika Vicoty Cherkemai (Kenya), aliyetumia 1:14:20 na kujinyakulia Sh laki 5.
    Nafasi ya nne alishika Sherekith Nyawera (Kenya), nafasi ya tano alikuwa Jane Mwikal (Kenya), nafasi ya sita alishika Failuna Abdi (Tanzania), nafasi ya saba alikuwa Mary Naali (Tanzania), nafasi ya nane ni Catherine Lange (Tanzania), nafasi ya tisa ni Yunice Mutie (Kenya) na na fasi ya kumi ni Ludera Fida (Kenya).
    Akizungumza katika mbio hizo, mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, alisema aliwapongeza waandaaji wa tukio hilo la aina yake.
    “Nawapongeza sana wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager, waandaaji na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja mmefanikisha mbio hizi kwa miaka 13 sasa,” alisema.
    Pia aliwapongeza GAPCO kwa kudhamini mbio za walemavu pamoja na wadhamini wengine ikiwemo Grand Malt, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,  CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA, Kilimanjaro Water, pamoja na wadhamini shirikishi wapya kabisa katika  mbio hizi ambao ni NSSF na Tanzania Coffee Board.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FABIOLA ACHUKUA DHAHABU KILI MARATHON 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top