• HABARI MPYA

    Monday, March 02, 2015

    OMOG NA SHIKANDA WATIMULIWA AZAM FC, GEORGE ‘BEST’ NSIMBE BOSI MPYA CHAMAZI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MCAMEROON Joseph Marius Omog (pichani kushoto) amefukuzwa kazi Azam FC pamoja na kocha Msaidizi namba mbili, Mkenya Ibrahim Shikanda, BIN ZUBEIRY imeipata hiyo.
    Omog amewapigia simu baadhi ya wachezaji na kuwaambia amefukuzwa kazi. Mmoja wa wachezaji wa Azam FC aliyepigiwa simu na Omog amesema; “Kocha kanipigia kaniaga, amesema amefukuzwa kazi,”.
    Omog anafukuzwa kazi baada ya Azam FC kutolewa katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na El Merreikh ya Sudan mwishoni mwa wiki.
    Azam FC ilianza vizuri kwa ushindi wa 2-0 nyumbani Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, lakini ikaenda kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano Khartoum.
    Pamoja na Merreikh ‘kubebwa’ na marefa, lakini Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC imejiridhisha mbinu za kocha huyo zilichangia timu kutolewa.
    Omog alianza kazi Azam FC Desemba 2013 akirithi mikoba ya Muingereza, Stewart John Hall na mwisho wa msimu huo, Mei mwaka jana akaiwezesha timu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya kwanza.
    Hata hivyo, katika msimu wake wa kwanza, Omog alishindwa kufikia rekodi ya Hall katika michuano ya Afrika, baada ya timu kutolewa Raundi ya Awali pia na Ferroviario de Nampula ya Msumbiji Kombe la Shirikisho.
    Ikishiriki kwa mara ya kwanza michuano ya Afrika, Kombe la Shirikisho mwaka 2013, Azam FC ilifika Raundi ya Tatu na kutolewa FAR Rabat ya Morocco, baada ya kuzitoa timu za Al Nasr Juba ya Sudan Kusini na Barack Young Controllers ya Liberia.
    Hadi anafukuzwa, Omog ameiongoza Azam FC katika mechi 55 za mashindano yote, ikishinda mechi 30, sare 14 na kufungwa 11.
    Sasa, Mganda George ‘Best’ Nsimbe anakuwa kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC kumalizia msimu wa Ligi Kuu, wakati Bodi ya Ukurugenzi ikiwa katika mchakato wa kusaka kocha mpya.
    Jukumu la kwanza la Nsimbe aliyeajiriwa kama Msaidizi wa Omog Januari mwaka huu kutoka KCCA ya kwao, Uganda ni kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu.
    Hadi sasa, Azam FC inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu kwa pointi zake 27 za mechi 16, ikiwa nyuma ya vinara, Yanga SC wenye pointi 31 za mechi 16 pia.
    Nsimbe ataiongoza kwa mara ya kwanza Azam FC Jumamosi itakapomenyana na JKT Ruvu katika Ligi Kuu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    George 'Best' Nsimbe (kushoto) sasa atakaimu ukocha Mkuu wa Azam FC
     

    REKODI YA JOSEPH MARIUS OMOG AZAM
    Azam FC 3-0 Ruvu Shooting (Kirafiki, Azam Complex) 
    Azam FC 2-0 Spice Stars (Kombe la Mapinduzi)
    Azam FC 1-0 Tusker FC (Kombe la Mapinduzi)
    Azam FC 1-0 Ashanti United (Kombe la Mapinduzi)
    Azam FC 2-0 Cloves Stars (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Azam FC 2-3 KCC (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Azam FC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara)
    Azam FC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara)
    Azam FC 4-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Bara)
    Azam FC 1-0 Ferroviario de Beira (Kombe la Shirikisho)
    Azam FC 0-2 Ferroviario de Beira (Kombe la Shirikisho)
    Azam FC 2-2 Prisons (Ligi Kuu)
    Azam FC 4-0 Ashanti United (Ligi Kuu)
    Azam FC 4-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
    Azam FC 2-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Azam FC 2-1 Simba SC (Ligi Kuu)
    Azam FC 3-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    Azam FC 2-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Azam 0-0 Rayon (Kagame)
    Azam 4-0 KMKM (Kagame)
    Azam FC 2-2 Atlabara (Kagame)
    Azam FC 4-1 Adama City (Kagame)
    Azam FC 0-0 El Merreikh (3-4 pen, Kagame)
    Azam FC 0-3 Yanga SC (Ngao ya Jamii)
    Azam FC 3-1 Polisi (Ligi Kuu)
    Azam FC 2-0 Ruvu Shoot (Ligi Kuu)
    Azam FC 0-0 Prisons (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Azam FC 0-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Azam FC 0-1 Ndanda FC (Ligi Kuu)
    Azam FC 2-1 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Azam FC 3-1 Mtibwa Sugar (Kirafiki Chamazi usiku)
    Azam FC 2-3 Sc Villa (Kirafiki, Nakivubo, Kampala)
    Azam FC 0-1 URA (Kirafiki Kampala, Uganda)
    Azam FC 3-0 Vipers (Kirafiki Kampala, Uganda)
    Azam FC 0-2 KCCA (Kirafiki, Kampala, Uganda)
    Azam FC 2-2 Yanga SC (Ligi Kuu Bara)
    Azam FC 2-2 KCCA (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Azam FC 1-0 KMKM (Kombe la Mapinduzi)
    Azam FC 1-0 Mtende (Kombe la Mapinduzi)
    Azam FC 1-1 Mtibwa Sugar (Azam ilitolewa kwa penalti 7-6 Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Azam FC 1-0 Stand United (Ligi Kuu)
    Azam FC 3-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Azam FC 1-1 SImba SC (Ligi Kuu)
    Azam FC 0-1 TP Mazembe (Kirafiki Lubumbashi)
    Azam FC 2-2 ZESCO United (kirafiki Lubumbashi)
    Azam FC 0-1 Don Bosco (kirafiki Lubumbashi) 
    Azam FC 2-2 Polisi Moro (Ligi Kuu Bara)
    Azam FC 2-0 El Merreikh (Ligi ya Mabingwa)
    Azam FC 0-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Mlandizi)
    Azam FC 0-0 Prisons (Ligi Kuu)
    Azam FC 0-3 El Merreikh (Ligi ya Mabingwa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OMOG NA SHIKANDA WATIMULIWA AZAM FC, GEORGE ‘BEST’ NSIMBE BOSI MPYA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top