• HABARI MPYA

    Monday, March 02, 2015

    VITOTO VYA MALI VYABEBA NDOO YA U17 AFRIKA BILA KUPOTEZA HATA MECHI MOJA

    Na Mwandishi Wetu, NIAMEY
    TIMU ya Mali imetwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, baada ya kuifung Afrika Kusini mabao 2-0 usiku huu Uwanja wa Jenerali Seyni Kountche mjini Niamey, Niger.
    Baada ya sare ya bila kufungana kipindi cha kwanza, Siaka Bagayoko akafunga bao la kwanza dakika ya 67 kwa Eaglets.
    Amajimbos ilipambana kutaka kusawazisha, lakini jithada za Luvuyo Mkatshana na Eric Mayo hazikumsumbua kipa wa Mali, Alou Traore.
    Mali wakifurahia na taji lao la U17 Afrika baada ya kuifunga Afrika Kusini 2-0

    Mchezaji bora wa mechi hiyo, Aly Malle akafunga bao la pili zikiwa zimesalia dakika 12 baada ya kuwatoka mabeki wawili, kabla ya kumtungua kipa Mondli Mpoto kufuatia pasi ya Boubacar Traore.
    Hiyo ilikuwa fainali yao ya kwanza Amajimbos, wakati kwa Mali wao walikuwa washindi wa pili wa mwaka 1997 nchini Botswana baada ya kufungwa 1-0 na Mafarao wadogo kutoka Misri. Matokeo mazuri zaidi kwa Amajimbos kwenye mashindano haya miaka ya nyuma ilikuwa ni kushika nafasi ya nne mwaka 2005 nchini Gambia baada ya kufungwa na Ivory Coast walioibuka washindi wa tatu.
    Timu zote ziliingia kwenye fainali ya jana zikiwa hazijapoteza mechi na zinaungana na Guinea na Nigeria kwenda Fainali za Fainali za Kombe la Dunia za FIFA U17 nchini Chile Oktoba mwaka huu.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikuwepo tangu mwanzo katika michuano hiyo kama mmoja wa Makamisaa na anatarajiwa kurejea leo Dar es Salaam baada ya takriban wiki mbili za kukosekana nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VITOTO VYA MALI VYABEBA NDOO YA U17 AFRIKA BILA KUPOTEZA HATA MECHI MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top