• HABARI MPYA

    Monday, March 02, 2015

    YANGA SC WATUA DAR NA KUUNGANISHA BAGAMOYO MAWINDO YA KUUA MNYAMA MACHI 8 TAIFA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Yanga SC kilitua usiku wa jana Dar es Salaam na moja kwa moja kuunganisha Bagamoyo, Pwani kwenda kuweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya mahasimu, Simba SC Jumapili wiki hii.
    Yanga SC iliwasili ikitokea Botswana ambako ilikwenda kucheza mechi ya marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji BDF XI.
    Katika mchezo huo uliofanyika Ijumaa usiku, Yanga SC ilifungwa mabao 2-1, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani Dar es Salaam.
    Mrisho Ngassa kulia akizungumza na kocha Charles Boniface Mkwasa. Mchezaji huyo ataungana na wenzake kambini Bagamoyo leo baada ya kutatua masuala yake binafsi mapema

    Na baada ya kutua tu, kikosi kizima, kasoro mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kilielelekea Bagamoyo kwa kambi ya maandalizi ya pambano la watani.
    Ngassa anatarajiwa kuungana na wenzake leo, baada ya kuomba udhuru wa kushughulikia masuala yake binafasi mapema leo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WATUA DAR NA KUUNGANISHA BAGAMOYO MAWINDO YA KUUA MNYAMA MACHI 8 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top