• HABARI MPYA

    Tuesday, March 03, 2015

    YANGA YAGOMEA MECHI YA WANAJESHI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Yanga imeigeukia kwa sura ya mbogo Bodi ya Ligi Tanzania baada ya kuahirishwa kwa mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu na wakasisitiza kwamba hawatakuja uwanjani.
    Akizungumza na na waandishi wa habari leo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema wameshangazwa na mabadiliko ya kila kukicha ya ratiba ya ligi hasa mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu ambao walitakiwa waucheze kesho kwa mujibu wa ratiba yao.

    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Yanga SC Jerry Muro ameshangazwa na mabadiliko ya kila kukicha ya ratiba ya ligi 

    Muro amesema bodi ya ligi imeonyesha kwamba haitaki Yanga ifanikiwe katika kampeni zao za kombe la Shirikisho kwa kuitaka kuucheza mchezo huo Machi 11 ikiwa ni siku tatu kabla ya kushuka katika Uwanja wa Taifa kucheza na Plutinum ya Zimbabwe.
    "Ratiba tuliyonao inayonyesha kwamba kesho kulitakiwa tucheze dhidi ya JKT Ruvu lakini hawa wenzetu kwa matakwa yao wamebadilisha ratiba pasipo kutuhusisha hii kwetu tunaichukulia kama hujuma,"amesema Muro.
    "Tumewaambia tangu jana kama wameufuta mchezo wa kesho na badala yake wakaupeleka Machi 11 Yanga hatutakuja uwanjani kwakuwa huo sio uzalendo hatuwezi kuacha maandalizi ya mechi yetu ya kimataifa kuangalia mechi ya ligi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAGOMEA MECHI YA WANAJESHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top