• HABARI MPYA

    Thursday, April 02, 2015

    MALINZI AWAAMBIA YANGA WASIBWETEKE NA 5-1 ZAO ZA TAIFA, WAKAKAZE ZIMBABWE

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewataka wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki kwenye michuano ya Afrika, Yanga SC kutobweteka.
    Kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (C2) dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe utakochezwa Jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo, Malinzi amewatakia kila heri Yanga SC.
    Malinzi amesema Yanga SC hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1 wiki mbili zilizopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.

    Endapo Yanga itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWAAMBIA YANGA WASIBWETEKE NA 5-1 ZAO ZA TAIFA, WAKAKAZE ZIMBABWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top