• HABARI MPYA

    Wednesday, April 01, 2015

    MICHO AONGEZA MKATABA WA MIAKA MITATU UGANDA, NI WIKI MOJA BAADA YA KUCHINJA TAI NIGERIA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Uganda limemuongezea Mkataba wa miaka mitatu, kocha wa zamani wa Yanga SC, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ kuendelea kuifundisha timu ya yaifa, The Cranes.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Uganda, Micho ambaye wiki iliyopita aliwaongoza Korongo wa Kampala kumchapa Tai wa Nigeria 1-0 nyumbani kwake, amesema kwamba ameongeza Mkataba wa miaka mitatu.
    “Nimeongeza Mkataba wa miaka mitatu kuendelea kufundisha Uganda. Najisikia kama nipo nyumbani. Naipenda Uganda na nawaahidi Waganda nitaongeza ufanisi ili kuwapa furaha wajivunie timu yao,”amesema Micho aliyezaliwa Septemba 1, mwaka 1969.
    IMG_6743
    FUFA imemuongezea Mkataba wa miaka mitatu kocha Milutin ‘Micho’ Sredojevic 
    Micho ataendelea kufanya kazi Uganda kwa miaka mitatu zaidi

    Micho kuongeza Mkataba Uganda kunavunja matumaini ya klabu yake ya zamani, El Hilal iliyokuwa inamuwania kumpata tena.  
    Uganda ni timu ya pili ya taifa kwa Micho kufundisha, baada ya Rwanda alikofanya kazi kati ya Novemba 1, mwaka 2011 na Aprili 17, mwaka 2013, kabla ya Mei mwaka 2013 kutua The Cranes.
    Micho mzaliwa wa Prokuplje, Serbia zamani Yugoslavia, kabla ya kuwa kocha amewahi kucheza soka akiwa mshambuliaji na timu alizochezea ni Olimpija Ljubljana, Svoboda Ljubljana, Sinđelic Belgrade, Graficar Belgrade, FK Zorka Subotica na FK Pionir Subotica zote za Serbia.
    Baada ya hapo, mwaka 1994 alianza kufundisha soka katika klabu ya FK Palic, kabla ya 2001 kuhamia FK Spartak Subotica na baadaye mwa mwaka huo, akachukuliwa kufundisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yugoslavia.
    Baadaye mwaka huo huo, 2001 akahamia FK Hajduk Kula, kabla ya mwaka 2001 alipohamia Afrika, ambako klabu yake ya kwanza kufundisha ilikuwa SC Villa ya Kampala, Uganda hadi 2004 alipohamia St George ya Ethiopia, alikodumu hadi 2006 akahamia Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
    Mwaka 2007 akatua Yanga SC ya Dar es Sakaam, Tanzania kabla ya baadaye mwaka huo kurejea St George alikopiga kazi hadi 2011 akatua El-Hilal ya Sudan- hiyo ikiwa klabu ya mwisho kufundisha kabla ya kwenda Rwanda na sasa Uganda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHO AONGEZA MKATABA WA MIAKA MITATU UGANDA, NI WIKI MOJA BAADA YA KUCHINJA TAI NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top