• HABARI MPYA

    Thursday, April 02, 2015

    RAHEEM STERLING: SI FEDHA, MATAJI YANANIKIMBIZA LIVERPOOL

    MSHAMBULIAJI Raheem Sterling ameonyesha yupo karibu kuondoka Liverpool baada ya jana kusema aligoma na hayuko tayari kusaini Mkataba mpya Anfield, kwa sababu kiu yake ni mataji na si fedha.
    Sterling amepewa ofa ya mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki ili abaki Merseyside na amesema katika mahojiano na BBC jana kwamba angekuwa amekwishasaini si chini ya mwaka mmoja uliopita.
    Lakini katika mahojiano hayo ya TV ambayo Liverpool haikuwa na inajua chochote kabla ya muda mfupi kuelekea kurushwa hewani, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amesema amekerwa kuhusishwa na kuhamia Arsenal – ambao watamenyana na klabu yake, Liverpool Jumamosi katika Ligi Kuu ya England – na kwamba ndoto zake ni kucheza nje.

    Raheem Sterling amekataa kusaini Mkataba mpya Liverpool baada ya kusitisha mazungumzo ya Mkataba hadi mwishoni mwa msimu

    RAHEEM STERLING MSIMU HUU 

    LIGI KUU ENGLAND 
    Amecheza mechi 28
    Amefunga mabao 6
    Ametoa pasi za mabao
    LIGI YA MABINGWA/ EUROPA LEAGUE
    Amecheza mechi 8
    Hajafunga bao  0
    Ametoa pasi ya bao 1
    Liverpool imekasirishwa na kitendo cha Sterling kuamua kufanya mahojiano bila hata kutoa taarifa kwa klabu na tayari baadhi ya Wajumbe wa bodi wanashawishika kwamba mwanasoka huyo wa kimataifa wa England na wawakilishi wake wanafanya mipango ya nkuondoka mwishoni mwa msimu.
    "Si kuhusu fedha hata kidogo," amesema Sterling. "Haijawahi kuwa kuhusu fedha. Nazungumzia kushinda mataji katika wakati wangu nikiwa kazini. Hicho ndicho nachokizungumzia. Sizungumzii nitakwenda kuendesha magari mangapi, nyumba ngapi nimepata. Nachotaka tu ni kuwa bora kadiri nitakavyoweza. 
    Sterling takes on Lithuania's Georgas Freidgeimas during England's Euro 2016 qualifier at Wembley
    Sterling akitafuta maarifa ya kumuacha beki wa Lithuania, Georgas Freidgeimas katika mechi ya kufuzu Euro 2016 akiichezea England Uwanja wa Wembley
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAHEEM STERLING: SI FEDHA, MATAJI YANANIKIMBIZA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top