• HABARI MPYA

    Wednesday, April 01, 2015

    SIMBA SC YAINGIA MKATABA WA MIAKA MITATU NA EAG, INAHUSU ‘MADILI YA KUPIGA FWEZA’

    Na Prince Akbar. DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya EAG Group Limited, imeingia Mkataba wa miaka mitano na Simba SC ambao utahusu kuitafutia dili klabu hiyo za kuingiza fedha.
    Mkurugenzi wa EAG, Imani Kajula ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mipango yote ya kuendesha dili hilo anaipata kutoka klabu ya Arsenal ya England, ambayo anafanya nayo kazi.
    Kajula amesema katika mkataba huo anataka kuona Simba inakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato, ili iache kutegemea mapato ya mlangoni na ada za wanachama pekee.
    Rais wa Simba SC, Evans Aveva (kushoto) akisaini Mkataba na Mtendaji Mkuu wa EAG Group Limited, Imani Kajula kulia leo Dar es Salaam
    Aveva na Kajula wakibadilishana fomu za Mikataba
    Mtendaji Mkuu wa EAG Group Limited, Imani Kajula (kushoto) akiwa na Meneja Maendeleo wa Arsenal, Daniel Willey (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo wa klabu hiyo ya England, Sam Stone kulia mwaka jana wakati akiingia Mkataba wa ushirikiana na klabu hiyo ya London. Kajula ameingia Mkataba wa miaka mitatu na Simba SC jana. 

    "Ukiangalia kwa sasa, mwakani Simba itafikisha miaka 80, lakini kiuchumi haiendani na hadhi hiyo. Sasa katika mkataba huu, tunataka kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa klabu kuwa na vyanzo vingi vya mapato,"alisema Kajula.
    Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema katika mkataba huo, wamepanga kutumia fursa hiyo kuendeleza mradi wao wa ujenzi wa Uwanja wao wa Bunju.
    Aveva pia amesema anaamini mpango huo utawawezesha kuendeleza jingo lao la makao makuu liliopo Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAINGIA MKATABA WA MIAKA MITATU NA EAG, INAHUSU ‘MADILI YA KUPIGA FWEZA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top