• HABARI MPYA

    Wednesday, May 20, 2015

    KOPUNOVIC AKUBALI KUSHUSHA DAU AENDELEE NA KAZI SIMBA SC, LAKINI MBELGIJI NAYE ANATUA DAR KESHO

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    HATIMAYE kocha Mserbia, Goran Kopunovic (pichani juu) amekubali kurejea Dar es Salaam kuendelea na kazi Simba SC.
    Tayari Simba SC ilikuwa imekwishakata tamaa na Mserbia huyo, baada ya kushindwa kutoa msimamo wake hadi Ijumaa kama atakubali ofa aliyopewa kusaini Mkataba mpya au la.
    Goran alishindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Simba SC juu ya Mkataba mpya, kutokana na kutaka kiwango cha fedha ambacho klabu iliona ni kikubwa.
    Goran Kopunovic amekubali kurudi kazini Simba SC

    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe aliiambia BIN ZUBEIRY wiki iliyopita kwamba Kopunovic alitaka dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la kusaini Mkataba na dola 8,000 (Sh. Milioni 16).
    Mwishoni mwa wiki, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akasema kwamba hawajapata jibu lolote kutoka kwa Kopunovic kama alivyoahidi angewajibu Ijumaa, hivyo wanaelekeza nguvu zao katika kusaka mwalimu mwingine.
    Lakini sasa inagundulika Kopunovic, aliyeiongoza 
    Simba SC katika mechi 24 tangu aanze kazi Januari mwaka huu kati ya hizo, timu imeshinda mechi 18, sare mbili na kufungwa nne, amekubali kurudi kazini Msimbazi.
    Sasa Mserbia huyo atarejea nchini kuanzia wiki ijayo kusaini Mkataba mpya na mara moja kuanza maandalizi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
    Mbelgiji Piet de Mol aliyekuwa anawania kurithi mikoba ya Goran, naye atakuja kama alivyopanga kesho, lakini kutafuta kazi klabu nyingine.
    Piet de Mol anatarajiwa kuwasili nchini kesho kusaka timu

    Kuna uwezekano, de Mol mwenye umri wa miaka 60 na uzoefu mkubwa wa kufundisha soka Afrika, Asia na Ulaya akaenda kujaribu bahati yake Mtibwa Sugar.
    Mwaka jana, Piet de Mol alikuwa nchini Ghana akifanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi
    Mbali na Ghana ambako alifanya kazi na Asante Kotoko, De Mol amefundisha timu pia kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na China. Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOPUNOVIC AKUBALI KUSHUSHA DAU AENDELEE NA KAZI SIMBA SC, LAKINI MBELGIJI NAYE ANATUA DAR KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top